JUNSI YA KUFUNGUA BLOG NA KUANZA KUINGIZA PESA NDANI YA MWEZI WA KWANZA.


UTANGULIZI:

Mara nyingi watu huwa wanajiuliza kuhusu jinsi bloggers wanavyoingiza mkwanja kupitia blog zao, ni ngumu kuelewa kwa watu ambao sio watundu wa internet lakini kwa wajanja ni ishu simpo sana.

hebu tufuatane hapa katika maelezo yangu nikupe mchongo mzima unavyokuwa kuhusu bloggers na jinsi ya kuingiza mkwanja kupitia blog yako,  ili uweze kunufaika na hii taarifa yangu lazima uwe blogger au unampango wa kuanzisha blog.

watu wengi huanzisha blog kwa kusikia kuwa watu wengine wameanzisha blog na zinawalipa, lakini sio jambo rahisi kabisa kuanzisha na kuendesha blog. ili uweze kunufaika na blog yako,lazima kwanza uwe tayari kuinvest nguvu, mali, akili na muda lukuki, sio rahisi kuanzisha blog leo halafu kesho ukategemea itaanza kukulipa, ni kitu kinachochohitaji subra kidogo na kujitoa kuhakikisha unayapata masikio na macho ya watu wanaopendezwa na contents za blog yako.

Sasa nisiwachoshe sana ngoja niingie kwenye mchongo wenyewe,

ukiwa tayari umeanzisha blog yako kwanza hakikisha unazingatia yafuatayo ili uweze kukamata akili na fikra za watu katka blog yako ambao ndio watakua soko kwako kwani utaingiza fedha kutokana na wao, nitakueleza mbele ya safari ni kwa nini wanaotembelea blog yako ndio wanaokupa mchongo wa pesa.

ZINGATIA:

Mwonekano wa blog yako. , hili ni suala la msingi sana wadau, hebu nikuulize kitu kimoja: wewe unapenda kukaa kwenye nyumba nzuri au mbaya? lahasha najua utapenda kukaa kwenye nyumba nzuri, hivyo hivyo na kwenye blog yako, wanaofuatilia blog yako au wanaopenda kusoma posts za blog yako watavutiwa kusoma kila mara posts zako kutokana na uzuri na mvuto wa blog yako. Hivyo hakikisha unaitengeneza blog yako kwa namna ambayo itakupendeza wewe mwenye pamoja na wasomaji wako ambao ni product muhimu sana kwako wewe blogger.

2. Mpangilio, hiki pia ni kitu kingine muhimu sana kwa bloggers, unapokuwa umeitengeneza blog yako, kupitia blogger templates au wordpress unatakiwa utumie template nzuri ambayo inaonekana vizuri kupitia simu na computer. hakikisha hiyo template ina mpangilio mzuri wa gadgets na widgets ili blog yako iwe na ubora mkubwa zaidi. Nikupe mfano mmoja, kama unatokea Dar es salaam, Mtaa wa manzese au magomeni au jangwani unafanana na oysterbay au masaki? lahasha haifanani kabisa na hiyo mitaa kama oysterbay, unajua kwanini? Mpangilio wa majengo na miundombinu mingine. Chukua huo mfano kisha hamishia kwenye blog yako, ukiwa na blog ambayo haina mpangilio mzuri itakua haina mvuto machoni pako wala kwa wasomaji wako, blog yako itakua kama magomeni au manzese.

3. Ubora wa unachokisambaza na maelezo ya kutosha, hapa msomaji wangu najaribu kukuelekeza kuhusu kile unachokiandika au unachopakia kila siku katika  blog yako,  jaribu kuwa mbunifu katika kila unachokiandika kiwe na mvuto ambao utamlazimu mtu mwingine anayesoma yaliyomo katika blog yako asome bila kuchoka. Pia epuka kutumia lugha zisizoeleweka maana mwisho wake ni kuwapoteza wasomaji wako.

4. Jina la blog yako, mara nyingi tunapokuwa tunaanzisha blog huwa hatujakusudia kuwa na mafanikio pengine, lakini ni vizuri kwa anayeanzisha blog kwa kulenga mafanikio flani, sio lazima yawe ya kifedha tu, bali hata kuwafikia watu wengi kwa mara moja ni mafanikio makubwa sana. Jina la blog yako na maelezo ya ziada ya blog yako ni muhimu sana kwani husaidia kukutambulisha wewe ni nani na blog yako inahusiana na nini. ni jambo baya endapo mtu atatembelea blog yako halafu jina unalotumia haliendani na kile ambacho unakipost katika kurasa zako kila siku. kwa mfano blog yangu mimi inaitwa shilingiyetu blog na pia inamaelezo ya ziada kwamba inahusika na siasa, michezo, habari za kitaifa na mambo madogo madogo mengine hivyo ni rahisi kwa mtu kuelewa ninachoandika kila siku. Ila kama wewe utapuuzia jina la blog yako ukaona halina maana katika kutambulisha blog yako hautakuwa serious na unachokifanya.

5. Lugha unayoitumia, kama blog yako ipo katika mazingira ya watu wanaotumi lugha fulani, huna budi nawe kutumia luha ile ile wanayotumia wasomaji wako, huwezikuwa unaendesha blog kwa lugha fulani ambayo haitumiwi na wasomaji wako, blog yako itakuwa ya kujifurahisha na haitakuwa na maana yoyote kwani hutakuwa na wasomaji.
          mfano, blog inayoendeshwa kwa kiingereza hapa Tanzania ni ngumu sana kupata wasomaji wengi kwani watanzania wengi wanatumia kiswahili kwa hiyo kama we ni blogger wa kiingereza jipange sana vinginevyo itabidi ufute blog yako au ubadilishe lugha. Sio mbaya kutumia lugha mchanganyiko, lakini kila unapotumia lugha fulani hakikisha unalilenga lile kundi wanaotumia lugha hiyo. Na kwa bahati kubwa, kwa sasa unaweza ukaweka gadget au kitufe cha TRANSLATION katika blog yako ili kila mtu apate tafsiri ya kile ulichokiandika kwa lugha yake.

6. Tambua wanachokipenda wasomaji wako, nikupe mfano mmoja, kama umelenga blog yako iwe ya habari basi lenga watu ambao wanapenda habari, watu wengine watajiuliza utajuaje hao watu wanapenda habari? ni vizuri kujiuliza hivyo, ila ni rahisi tu kuwapata. kwa kuwa blog husambaza au kushare habari kupitia mitandao ya kijamii kama facebook, twitter, google+ na kadhalika, mimi nitatolea mfano mtandao wa facebook.
               tafuta makundi ya facebook yanayohusu habari, kisha utakuwa unayatumia katika kusambaza habari zako, huko utawakuta wapenda habari kibao na watakuwa wafuasi wako pia. utafanya hivyo kwa kila unachokiandika na kukielekeza kwenye makundi ya mitandao ya kijamii na huko utapata wafuasi kibao.

7. Penda kutembelea blog za watu wengine ambazo zimeendelea kuangalia zilivyo ili na wewe uweze kurekebisha blog yako. kwa lugha ya kiingereza tunaita "mentor", maana rahisi ya neno hili ni mtu anayekuongoza au kukupa mwongozo. simaanishi awe anakuongoza kile cha kufanya, hutakuwa huru sasa katika blog yako, namaanisha blog utakayokuwa unaifatilia au utakazozifatilia kuona zinaendeshwaje?
ikiwezekana unaweza kuunganisha mawasiliano yako kwa wale waongoza blog kwa maelezo mbalimbali kama watakuwa tayari kukusaidia. mimi napenda ufanikiwe kwenye blog yako hivyo ukivutiwa na msaada wangu fuata blog yangu shilingiyetu blog nikupe msaada.

JINSI YA KUTENGENEZA PESA MTANDAONI:

Hebu nisikilize kwa makini sana hapa nikupe mchongo wa maana kabisa, kama ulikuwa unasoma hii kitu halafu unasikiliza muziki hebu zima sasa alafu punguza sauti ya tv au redio hapo pembeni, halafu kama una
glass ya juis au maji itakuwa vizuri pia ili tusafiri kwa pamoja kwa muda mrefu na kinywaji chako hapo pembeni nikupe mchongo.

Pesa mtandaoni kwa kiasi kikubwa zinatokana na matangazo ambayo huwa yanasambazwa na kampuni za matangazo na masoko mtandaoni. ambapo matangazo hayo husambazwa katika websites na blogs mbalimbali kwa ruhusa ya wenye blogs au websites.

endapo mmiliki wa blog ataweka matangazo ya kampuni za matangazo kama hizo hapo chini, basi ataweza kuingiza pesa kutokana na CLICKS za wasomaji wa blog au website yake katika matangazo hayo, pia kutokana na ACTIONS, hii ni pale msomaji wako akinunua bidhaa au kudownload chochote kutokana na tangazo la kampuni lililopo kwenye blog au website yako wewe mmiliki wa hiyo blog au website unagawio lako katika hiyo download. pia makampuni mengine hulipa kutokana na IMPRESSION,    impression maana yake ni ile hali ya msomaji wko kufungua na kukuta tangazo au kuona tangazo katika blog au website yako kwako inakuwa ni pesa.


ZIPO NJIA ZITUATAZO KUTENGENEZA PESA  MTANDAONI

1. Adsense hii ni njia moja wapo ambayo hutumiwa na bloggers wengi kimataifa katika kuingiza pesa kupitia blog zao. njia hii ni nzuri lakini sio rahisi kufanikiwa, inahitaji qualifications nyingi kuliko hata zile za kuingia chuo kikuu ( natania tuh) ila maana yangu kubwa ni kwamba njia hii ni ngumu maana ili ufanikiwe kuonyesha Ads (matangazo mbalimbali ya google) unatakiwa kwanza kufungua account ya googleadsense ambayo lazima ichunguzwe kisha wao wenyewe wataruhusu na kuithibitisha itumike, hatua hii ya kufungua account na kusubiri approval inaweza kuchukua hadi mwezi mmoja na kuendelea kutokana na mahali ulipo. sehemu kama india huweza kuchukua hadi miezi sita kufanikiwa account kuwa approved lakini hapo huwa bado kabisa kufikia ndoto yako ambayo huwa ndoto ya bloggers wengi kuonyesha matangazo ya google kwenye blog zao.


2.Revenue hits njia hii imekuwa bora kwangu maana hata mimi ninaekuandikia data hizi huwa ninaitumia, na inanisaidia kuingiza mkwanja, unaanza kwa kufungua account kisha unasubiri approval, ndani ya siku mbili account yako iankuwa tayari unaanzz kutengeneza au kuchagu aina ya ads zitakavyokuwa zinaonekana kataka blog yako. baada ya hapo unaweza kutengeneza adcode, baada ya kutengeneza adcode unaenda kwenye blog yako una login alafu unaenda kwenye template uaningia kisha unachagua edit HTML na unazi paste au kuziweka zile adcode ulizo copy kwenye account yako baada ya ku create hizo adcode. kuanzia hapo utaanza kuona matangazo kataka blog yako ambayo yatakuingizia kipato, jinsi ya unavyoingiza kipato kwenye Revenue hits hutegemea na idadi ya watu wanaotembelea blog yako na kuona kurasa za matangazo ya Revenue hits, endapo msoji wako ataingia kwenye tangazo hilo kwa ku click, impression, au action wewe mwenye blog unapata kiasi cha fedha, au endapo msomaji wako atadownload chochote kupitia tangazo lililopo kwenye blog yako wewe mwenye blog uanaingiza pesaImage result for REVENUE HIT
3. zhakkas ads market, hii pia ni njia nzuri sana kwa bloggers wanaoanza na ambao hawaweza kuwa traffic kubwa, traffic ni idadi ya wanaotembelea blog yako. kama wewe ni newbie blogger yaani unayeanza basi hii ni poa sana kwako maana itakufanya utengeneze pesa kiulaini kabisa bila wasiwasi. haina mlolongo mrefu, hii nayo utatakiwa kufungua account ya zhakkas ili uanze kutengeneza adcode na kuzihamishia kwenye blog yako katika  HTML za blog yako. Utauliza unazipataje hizo html, vizuri kwa swali lako. Jinsi ya kuzipata ni rahisi sana, unachotakiwa kufanya login kwenye blog yako halafu tafuta template na ifungue, ukishafungua utaona edit HTML ingia kwenye hizo HTML na uziweke zile adcodes ulizopata kutoka kwenye account yako ya zhakkas, baada ya hapo utaanza kuona matangazo ya zhakkas kwenye blog yako. utaingiza pesa kama nilivyokuelekeza katika njia ya hapo juu. zhakkas wanakulipa kutokana na shughuli mbalimbali za watembeleaji wako kama clicks, impression na action. endapo mtu atatembelea ukurasa wako basi hapo atakuwa amefanya impression hivyo wewe utalipwa, aki click au kubofya tangazo lao we unalipwa na akidowload au kupakua wewe unalipwa simple kabisa.


4.Adsoptimal hii hapa tena nyingine ndugu, pata mkwanja kama we ni blogger, usiangalie utaanza kupata shilingi ngapi, mwanzo ni mgumu utaanza kwa pesa za vocha lakini baadae unafanikiwa kama bloggers wengine wanaoingiza mpaka mamilioni kwa kazi ya bloging only, naskia raha sana kuandika mambo haya, vijana hii ndo michongo ambayo haihitaji shida sana yaani ni wewe tu unagonga pesa mpaka unachanganyikiwa. utaratibu wake unafanana tu na taratibu za njia hizo zilizotangulia. ingia hapa uanze kuingiza mkwanja sign up

Kwa watakao hitaji website/blog  
0714183611 - website/blog designer

No comments:

Post a Comment